Waziri wa Afya, Maendeleo, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amezungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Afya na Ukimwi wa SADC.
Waziri Ummy amesema Tanzania itatumia mkutano huo kutangaza shughuli za Bohari ya Dawa (MSD) ambayo ilishinda zabuni ya kufanya Ununuzi wa pamoja wa dawa, vifaa na vifaa tiba kwa nchi za SADC.
Pia mkutano huo utajadili afya ya uzazi,mama na mtoto kwa kuangalia namna ya kupunguza vifo vya akina mama wajawazito, chanjo kwa watoto na kuimarisha afya kwa wasichana balehe.
MISS WORLD AINGIA TANZANIA KWA MARA YA KWANZA, WAZIRI KUFIKISHA UJUMBE KWA MAGUFULI