Club ya Arsenal usiku wa October 30 2019 ilikuwa Anfield kucheza mchezo wao wa Carabao Cup dhidi ya wenyeji wao Liverpool, Arsenal katika mchezo huo walionekana kuwa na kiwango cha juu na kufunga magoli ya uongozi mara kadhaa lakini nidhamu yao ya ulinzi iliyafanya yarudi kwa haraka.
Arsenal ilipewa nafasi zaidi ya kupata ushindi katika mchezo huo kutokana na kutumia wachezaji wake wengi wa kikosi cha kwanza, mchezo huo uliomalizika kwa dakika 90 sare ya kufungana kwa magoli 5-5 lakini Liverpool katika hatua ya mikwaju ya penati wakashinda kwa penati 5-4 na kutinga robo fainali ya michuano hiyo.
FT:Liverpool 5-5 Arsenal (Shkodran 6’O.G Milner 43’P Chamberlain 58′ Origi 61′ 90+4′) (Torreira 19′ Martinelli 26′ 36′ Maitland 54′ Willock 70′)
Liverpool wanafuzu kucheza robo fainali ya Carabao Cup kwa kuitoa Arsenal katika ushindi wa penati 5-4 #MillardAyoSPORTS pic.twitter.com/Ise5qu3G7R
— millardayo (@millardayo) October 30, 2019
Wengi wanahoji Arsenal licha ya kushusha kikosi chao kilichokuwa na wachezaji wengi wa kikosi chao cha kwanza ukilinganisha na Liverpool iliyokuwa na wachezaji wengi wa timu zao za vijana, wanaonekana kuwa na tatizo la kuongoza na baadae kuruhusu kirahisi timu pinzani kusawazisha.
AUDIO: Edo Kumwembe aeleza kocha anaestahili kuwa Yanga sio Zahera