Club ya Yanga SC imemaliza safari yake ya michuano ya kimataifa usiku wa November 3 2019 nchini Misri baada ya kucheza mchezo wake wa marudiano wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la shirikisho Afrika.
Yanga SC waliingia katika uwanja wa 30 June kurudiana na Pyramids wakiwa nyuma kwa magoli 2-1, magoli ambayo yalifungwa katika mchezo wa kwanza jijini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Yanga kwa kipigo cha 3-0 kinawaondoa rasmi katika michuano hiyo kwa aggregate ya 5-1
Kufunga magoli mawili bila kuruhusu kufungwa goli imekuwa ngumu zaidi na kujikuta wakimaliza mchezo huo kwa kupoteza kwa kufungwa kwa magoli 3-0 , magoli ya Pyramids FC yakifungwa na Traory dakika ya 27, Farouk 79 na El Said dakika za nyongeza, kwa maana hiyo Tanzania sasa msimu wa 2019/20 haina muwakilishi yoyote wa kimataifa katima michuano hiyo.
VIDEO: Mpoki alivyomvunja mbavu Rais Mstaafu Kikwete