Beki wa Club ya Simba SC Shomari Kapombe ameamua kutangaza rasmi kuwa ameandika barua ya kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, licha ya kuwa umri wake bado unaruhusu kuendelea kuitumikia Taifa Stars.
Kapombe ametangaza kufikia hivyo baada ya kutathmini afya yake, kwani anadai Taifa Stars inahitaji wachezaji watakao kuwa fiti kwa asilimia 100 na upande wake haoni kama anaweza kujitoa kwa asilimia 100 kwa sababu amekuwa akikimbwa na majeraha, hivyo kaomba aendelee kuitumikia timu yake ya Simba SC ambayo haina mashindano mengi zaidi ya Ligi.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Shomari Kapombe toka aumie mwishoni mwa mwaka 2018 akiwa nchini Afrika Kusini katika kambi ya Taifa Stars kujiaandaa na mchezo dhidi ya Lesotho wa kuwania kufuzu AFCON 2019, amekuwa na majeraha ya sio isha, hivyo ameona apumzike akiwa fiti atarudi.
Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo ameonesha sehemu ya maandalizi yake kuelekea pambano lake la kihistoria dhidi ya bondia wa kiphilipino Arnel Tinampay kutoka kambi ya Manny Pacquiao, Mwakinyo anajifua kupambania kuendeleza rekodi ya kuwapiga wapinzani wake KO Novemba 29 lakini Arnel hajawahi kupoteza kwa KO.
VIDEO: Mpoki alivyomvunja mbavu Rais Mstaafu Kikwete