Chama cha ACT Wazalendo kimesema kuwa Wagombea wake zaidi ya 2000 wameenguliwa bila kufuata utaratibu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa huku wakidai kuwa Chama cha Mapinduzi CCM wagombea wao wamepoteza sifa za kugombea kwakua walipitishwa kwa ngazi ya Tawi huku kanuni ikitaka wapitishwe kwa ngazi ya chini ambayo ni shina.
Kaimu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Dorothy Semu amesema Kamati ya uUongozi ya ACT Wazalendo itakaa kikao cha dharula kesho Ijumaa kutafakari hatua za kuchukua iwapo wagombea wao hawatorudishwa kugombea.