Leo November 8, 2019 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Nchini (ATCL), Ladislaus Matindi amesema kuwa wao hawachagui Wanawake kwa ajili ya kuwapeleka kuonesha uzuri kwenye ndege bali kuna vigezo vya mtu kuwa mhudumu.
Amesema, wanapimwa uelewa, kujua wana uwezo upi wa kufuatilia mafunzo watakayopewa ili watoe huduma inayotakiwa kwa wateja na sio kuangalia sura.
Majibu hayo yanakuja kutokana na Mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Husna Mwilima kudai Wahudumu wa Ndege za ATCL hawana mvuto kwa wateja.