Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ameendelea kusisitiza kauli yake ya kuwatembezea bakora wale wote wanaosema Serikali haijafanya maendeleo yoyote tangu Nchi ilipopata uhuru na kwamba huwa hatanii.
Ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza na wananchi wa Kata ya Utengule- Usangu Wilayani Mbarali baada ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata hiyo ambacho kinajengwa kwa zaidi ya shilingi milioni 400.
Amesema kuna baadhi ya watu wanastahili kucharazwa bakora ili waone maendeleo yaliyofanywa na Serikali ikiwemo katika Sekta ya Afya, Elimu na Miundombinu ya barabara ambayo imejengwa kwa fedha nyingi.