Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeteketeza zaidi ya mifuko mbadala Milioni mbili iliyotengenezwa chini ya kiwango na kiwanda cha Jin Yuan Investment kilichopo Jijini Mwanza na gunia nane ya vifungashio viliyoingizwa nchini kwa njia za magendo.
Akizungumza mara baada ya kufanya zoezi la uteketezaji wa mifuko hiyo Jijini Mwanza, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Samuel Gwamaka amesema zoezi hilo liwe onyo kwa wazalishaji wengine ambao hawafuati utaratibu na kanuni za viwango zilivyoweka za 70 gsm ili kulinda soko la ndani la bidhaa hizo.
“Lengo letu ni kulinda viwanda vya ndani ili vipande masoko ya bidhaa wanazozalisha lakini imekuwa ni kinyume kwa wawekezaji kuzalisha mifuko iliyochini ya kiwango cha gsm 70 ambayo imepitishwa na Shirika la Viwango nchini(TBS),” Dkt.Gwamaka.
“Wazalishaji wakifuata sheria na viwango vilivyowekwa vya 70 gsm na kuweka nembo ya mzalishaji kwenye mifuko inayozalishwa nchini itasaidia kubaini mifuko iliyochini ya kiwango na kufanya wepesi kwa mamlaka kushukua hatua,” Dkt.Gwamaka