Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo, amemshukuru Rais Magufuli kwa kukubali mwaliko katika tukio la kihistoria katika Jeshi la uwekaji wa jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa Dodoma leo, ambapo amemwambia tayari Makao Makuu ya Jeshi yameshahamia Dodoma kwa muda.
“Ukamilikaji wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa utaongeza tija katika usimamizi na uongozi wa Ulinzi na Usalama wa Taifa letu unaokidhi mazingira na mahitaji ya zama hizi” – CDF Mabeyo
“Kwa sasa Makao Makuu ya Jeshi tayari sote tumehamia Dodoma kwenye Makao Makuu ya muda”-Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi.