Ukubwa wa jina lake pamoja na matukio yanayomuandama ndio unamfanya afatiliwe kwa karibu na kutengeneza stori kwa kila anachokifanya hata kama ni kitu cha kawaida.
Stori ya sasa ya Chris Brown ni maongezi aliyoyafanya na mpenzi wake aitwae Karrueche ambae wamekua wakiandikwa kwamba wameachana.
Breezy kwenye haya maongezi aliwashukuru mashabiki wake ambao wamekua wakimpa support wakati wa shida na raha ambapo baada ya kuwashukuru fans, kitu kilichobaki ambacho alisema ni muhimu ni kumwambia Karrueche kwamba anampenda.
Najua kwa wanaofatilia stori za Chris Brown hii ni kubwa kwao hasa kutokana na kusikia maneno mengi kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wa wawili hawa.
Tazama video fupi hapa chini..