Round ya tano ya michuano ya UEFA Champions League hatua ya makundi imeendelea tena kwa michezo kadhaa kuchezwa, Jose Mourinho akiwa na Tottenham Hotspurs yake wamefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora baada ya kufanya come back 2-0 na kupata ushindi wa 4-2 dhidi ya Olympiacos.
Spurs wanafuzu kwa kujihakikishia kumaliza nafasi ya pili nyuma ya FC Bayern Munich anayeongoza Kundi kwa point 15, Real Madrid na PSG baada ya kutoka sare ya 2-2 zote zinafuzu kucheza hatua ya 16, Real Madrid wakiwa nafasi ya pili kwa point 8 huku PSG akiongoza kwa point 13.
Ushindi wa 1-0 wa Juventus dhidi ya Atletico Madrid unaipeleka Juventus hatua inayofuata na licha ya Atletico kuwa nafasi ya pili kwa kuwa na point 7 atalazimika kusubiri hadi mchezo wake wa mwisho ili kujua hatma yake kwani FC Bayer Leverkusen aliyepo nafasi ya 3 ana point 6 hivyo bado ana nafasi nae, sare ya 1-1 nyumbani inamvusha Man City dhidi ya Shakhtar na Shakhtar kubaki na sintofahamu kwa kutakiwa kusubiri hadi mchezo wa mwisho ndio wajue hatma yao.
VIDEO: Samatta baada ya kupokea comments zinazodai hachezi vizuri Taifa Stars