Usiku wa December 4 2019 ikiwa zimesalia siku chache toka Jose Mourinho afutwe kazi na Man United kama kocha mkuu na nafasi yake kuchukuliwa na Ole Gunnar Solskjaer, Mourinho usiku wa December 4 ndio alirejea Old Trafford safari hii akiwa kama kocha wa Tottenham Hotspurs kucheza dhidi ya Man United.
Wengi wakiwa wanasubiri labda Mourinho kama ataondoka na ushindi atatoa kijembe au tambo gani Old Trafford, jambo hilo limeshindwa kutimia baada ya kujikuta Tottenham kufungwa kwa magoli 2-1, hivyo Mourinho akaondoka uwanja huo akiwa mnyonge tofauti na matarajio ya wengi kuwa anaweza kupata matokeo kwa Man United hii ya sasa inayosuasua.
Magoli ya Man United yalifungwa kwa ufundi mkubwa wa Marcus Rashford dakika ya 6 ya mchezo kabla ya dakika 48 kufunga la pili kwa mkwaju wa penati, licha ya Dele Alli kufunga mapema goli la kusawazisha dakika ya 38 lakini Tottenham walishindwa kusawazisha walau waondoke hata na point moja.
VIDEO:MKENYA ALIYEFUNGA SAFARI KUTOKA KENYA HADI OLD TRAFFORD KISA MOURINHO