Ruben Nasoro Mushi ni miongoni mwa wafungwa walioachiwa kwa msamaha wa Rais Magufuli katika Gereza la Karanga Moshi Mkoani Kilimanjaro baada ya kukaa jela kwa Miaka tisa, amesema alipelekwa Magereza kwasababu ya kumjeruhi Mke wake kwa kisu tumboni pamoja na kumkata na shoka kwenye paji la uso na kinachomfanya aogope kurudi nyumbani ni kwamba anamuhofia Mkewe huyo.
Ruben amesema anaogopa kurudi nyumbani kwa kuhofia kupewa kesi nyingine kwa kuwa Mke wake ameshampeleka Mtoto wake wa kumzaa Magereza kwa kosa la uharibifu wa mali.