Kampuni ya Uchimbaji Madini ya dhahabu ya Suleiman and Partners chini ya Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Suleiman Lucas imeahidi kuchangia Shilingi Milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kupeleka umeme katika Kata Silanga Wilayani Kaliua.
Hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa wananchi wa Kata hiyo wanapata huduma hiyo na kuiwezesha Kampuni hiyo kutumia umeme katika utekelezaji wa shughuli zake za uzalishaji.
Kauli hiyo imetolewa jana Wilayani Kaliua na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Suleiman Lucas wakati alipomuomba Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri kuwasaidia kuisisitiza TANESCO iwapelekee umeme.