Shughuli za kiuchumi na kijamii zimesimama jijini DSM nchini Tanzania majira ya Alfajiri leo Jumanne Desemba 17, 2019 kutokana na mvua zinazonyesha na kusababisha usumbufu kwa waendao kwa miguu na wenye magari jijini.
Mbali na barabara kujaa maji baadhi ya mifereji nayo imefurika huku ngurumo za radi zikisikika huku anga likiwa katika hali ya giza.
Kando ya barabara baadhi ya watu wameonekana wakiwa wamejikunyata wakisubiri huenda mvua hii kubwa iliyoanza kunyesha ghafla mapema leo itapungua ili waendelee na shughuli zao.
Hali hiyo ni mwendelezo wa mvua kubwa ambazo kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitoa angalizo kwa mvua kubwa kutokea kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma, Lindi, Mtwara na maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro.
AyoTV na millardayo.com inakusogezea video fupi fipi zinaonyesha athari ya mvua katika eneo la pembezoni mwa Shule ya Msingi Kibasila hapa ni karibu na Mataa ya Serengeti.