Serikali imesema inaendelea kuboresha huduma za Afya kwa kusogea huduma kwa Wananchi hivyo inatarajia kuanza ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Magharibi mkoani Tabora itakayo hudumia mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora
Ujenzi huo unatarajia kuanza mapema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Kusini mkoani Mtwara hii ni kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu baada ya kupewa nafasi ya kusalimia na RC Mwanri kwenye kikao ushirika mkoani Tabora
“Huduma zote zitakuwa zinapatikana Tabora tikimaliza kujenga Mtwara tunaanza ujenzi wa hospital ya kanda ya Magharibi mikoa ya Katavi,Kigoma watakuja hapa” Waziri Ummy
CHEREHANI GALA: SPESHOZ NA NAIBU WAZIRI MAVUNDE ALIPOKUTANA NA DESIGNERS