Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Nchini Tanzania, Mhandis Bruno Ching’andu, amewashukuru Marais kutoka nchi mbili zinazounganisha reli hiyo Ikiwa ni pamoja na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt John Magufuli, Rais wa Zambia Edger Lungu na Rais wa Zimbambwe, Emmerson Mnangagwa kwa kuwapa fursa ya kusafirisha mizigo wenye tani 17 za mahindi.
Mhandis Chin`gandu, ametoa shukrani hizo alipokuwa nchini Zambia katika stesheni ya New Kapiri Mposhi, alipokuwa akitoa tathimi ya usafirishaji wa tani hizo za mahindi zilizotokea Vyawa na Makambako nchiniTanzania kwendaBulawainchiniZimbambwe.
“Tumetumia jumla ya treni 16 Kusafirisha tani zote hizi 17 lakini endapo tungetumia malori, yangesafirisha malori 531 na pia kungekuwa na msongamano wa mabasi barabarani na kusababisha uharibifu wa barabara njiani kwa hiyo ni jambo la kushukuru sana kuwapo na rehi hii” amesema Mhandis Chin`gandu.
Aidha amesema lengo lao la kusafirisha mzigo huo ilikuwa ni kusafirisha kwa miezi mitatu, lakini wanamshukuru Mungu wamesafirsha kwa miezi miwili ambayo hawakutegemea.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Reli ya Zambia, Christipher Musondo amesema ni jambo zuri la nchi hizo kuungana kuwa na umoja na kusaidiana kijamii,na pia amesema nchi hizo zinapaswa kupata bidhaa nyingi za kusafirisha kwenda maeneo mengine kama Afrika ya Kusini hata DRC Kongo.