Rais Magufuli leo December 22, 2019 ameungana na Waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Chato Mkoani Geita kusali Dominika ya 4 ya Majilio na ametumia nafasi hiyo kuwatakia Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya Watanzania wote.
Katika salamu hizo, Rais Magufuli amesema tunapoelekea katika sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya Wakristo na Waumini wa Madhehebu mengine mbalimbali wanalo jukumu la kuendelea kuombea amani, upendo na umoja kwa wanadamu wote bila kubaguana.
“Niwaombe ndugu zangu wa Chato na Watanzania kwa ujumla, tusherehekee sikukuu ya Krismasi kwa amani na upendo mkubwa, lakini pia tuukaribishe Mwaka Mpya kwa amani na upendo mkubwa wa Kristo’ JPM
“Mwaka unaokuja uwe mwaka wa mafanikio, uwe mwaka wa maendeleo, uwe mwaka wa kujenga umoja wetu kwa Watanzania wote, uwe mwaka wa amani na upendo na uwe mwaka wa kuendeleza Taifa letu katika maendeleo ya kweli”-JPM
WAZIRI APIGA MKWARA, AITAKA BILIONI 1 “HUWEZI ACHIA NGAZI”