Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi wa kesi inayomkabili Mfanyabiashara Khamisi Luwonga anaedaiwa kumuua Mkewe Naomi Marijani kwa kumchoma kwa kutumia gunia mbili za mkaa umekamilika.
Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai hayo mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa, kesi imeahirishwa hadi January 07, 2020.
Mfanyabishara Khamis Saidy, anadaiwa kutenda kosa hilo Mei 15, 2019, nyumbani kwake maeneo ya Gezaulole Kigamboni, baada ya kumuua na kisha kumchoma moto wa magunia mawili ya mkaa mke wake na kisha kuyabeba mabaki ya mwili huo na kwenda kuyafukia shambani kwake Mkuranga.
MAPOKEZI YA MSHINDI WA BONGO STAR SEARCH MBEYA