Rais Magufuli ametoa siku tano kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Adolf Mkenda kuondoa tofauti zao vinginevyo atatengua uteuzi wao, ametoa kauli hiyo Leo Dec 31, 2019 akiwa Kisiwa ch Rubondo.
“Ninafahamu Watendaji wenu wa juu, Katibu Mkuu na Waziri Kigwangalla kila siku wanagombana na ninawatazama taratibu, nilishampa kazi Katibu Mkuu Kiongozi awaite awaeleze ila wasipobadilika nitawaondoa, siwezi kuteua Watendaji halafu kila siku wanagombana” – JPM
“Kuna mambo mengi hayaendi, Katibu Mkuu hamheshimu Waziri na Waziri (Kigwangalla) nae hataki kwenda na Katibu Mkuu, siwezi kuvumilia hilo” – JPM
“Kwahiyo nalizungumza hili siku ya leo December 31,2019 kwamba Waziri Kigwangalla na Katibu Mkuu wake wajirekebishe na ikiwezekana wajirekebishe ndani ya siku tano wawe wanasalimiana, wanazungumza, mimi nina fahamu nina vyombo ninajua nani hafai zaidi” – JPM
MGOGORO WA ARDHI KATI YA JIJI NA WANANCHI “TUNAOMBA RAIS MAGUFULI ATUSAIDIE”