TAKUKURU Mkoani Dodoma inatarajia kuwafikisha Mahakamani watuhumiwa wanne kwa makosa mbalimbali ya rushwa akiwemo James Kwangulija (27) Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa shahada ya kwanza ya Ualimu katika Chuo kikuu cha St. John.
Mwanafunzi huyo anakabiliwa na kosa la kujaribu kutoa hongo ya Tsh. laki tisa kwa Afisa Mitihani wa Chuo hicho ili aweze kusaidia kuongeza ufaulu (GPA) za wanafunzi wenzake sita kinyume na sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.
Mkuu wa TAKUKURU Dodoma Sosthenes Kibwengo amesema vitendo hivyo vinapelekea kuwa na wanafunzi ambao hawana uwezo, wanaotegemea kufaulu kwa kuhonga.