Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA Taifa, Halima Mdee amesema watahakikishawapigania maslahi ya wanawake na watoto kwa kushinikiza marekebisho ya Sheria ya Ndoa ili kupinga Ndoa za utotoni.
Halima Mdee ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini DSM.
“Kati ya watoto 5 wawili wanaolewa chini ya miaka 18, na wengi wao wanachukuliwa kuanzia miaka 8 mpaka 10 na hakuna anayechukua hatua, ndiyo maana ni kawaida kusikia Mwalimu kabaka wanafunzi wake 24“ Halima Mdee
“Kutokana na alilolianzisha Mwanaharakati Rebeka sisi BAWACHA tunaitaka Serikali kuleta mabadiliko ya Sheria ya Ndoa, ili kumnusuru mtoto wa kike“ Mdee