January 8, 2020 Gharama za mafuta ghafi zimepanda kwa 1.4% kwa dola 69.21 za Marekani kwa pipa moja zimepanda baada ya kambi mbili za Majeshi ya Marekani nchini Iraq kushambuliwa na makombora.
Televisheni ya Taifa ya Iran ilisema kuwa shambulio lilikuwa ni kisasi baada ya kuuawa kwa Kamanda wa Juu wa Jeshi la nchi hiyo Qasem Soleimani.
Shambulio lilitokea saa chache baada ya shughuli za mazishi ya Soleimani, aliyeuawa na shambulio la Marekani siku ya Ijumaa.
Hali hii inaelezwa inaweza kuathiri usafirishaji wa mafuta kupitia lango la Hormuz linalotenganisha Ghuba ya Uajemi na Ghuba ya Oman. Takriban moja ya tano ya mafuta duniani husafirishwa kupitia lango hilo linalounganisha eneo la Ghuba na Bahari ya Arabia.