Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda ya Magharibi mwishoni mwa mwaka 2019 wamefanya msako na kufanikiwa kukamata silaha nane na nyingine 29 kusalimishwa.
Katika msako huo silaha zilizokamatwa ni riffle 2, gobore 6, meno ya tembo vipande vinne yenye uzito wa Kilo 40, nyama ya twiga vipande 30, pofu vipande 25, nsya vipande 10, ngozi 1 ya sitatunga na watuhumiwa 15.