Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ameagiza kuwekwa ndani na kutolewa katika nafasi zao Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Tukuyu Manase Ngogo na Afisa Ugavi Vumilia Mwaijande kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wao.
Dkt. Ndugulile ametoa agizo hilo Wilayni Rungwe mkoani Mbeya wakati alipotembelea Hospitali ya Tukuyu na kujionea utendaji mbovu wa Hospitali hiyo katika kutoa huduma kwa wananchi.
Dkt.Ndugulile amegiza kukatwa na kuwekwa ndani kwa Mfamasia na Afisa Manunuzi wa Hospitali hiyo kutokana na usimamizi mbovu wa stoo ya dawa na kukosekana kwa taarifa sahihi za Dawa zinazotoka na zinazoingia katika stoo hiyo.
“Nilishapata taarifa za wizi wa dawa Tukuyu sasa hili linadhibitisha hilo, huwezi ukamuweka Afisa Ugavi asimamie stoo ya Dawa wakati Mfamasi yupo” Dkt. Ndugulile
Aidha Dkt. Ndugulile amesikitishwa na utendaji mbovu wa Hospitali hiyo usiozingatia maelekezo ya Wizara katika uendeshaji wa Hospitali katika maeneo tofauti ya utoaji huduma.
Dkt. Nduguile amewapa onyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, muuguzu Mkuu wa Wilya na Mfamasia wa Hospitali na kuwataaharalisha na utendaji wao wa akzi kwani umekuwa sio wa kuridhishwa na ameahidi kuwangalia kwa karibu zaidi.
“Katika ziara zangu zote sijawahi kuona utumbo kama huu niseme tu sijaridhishwa na utendaji wenu kabisa na Mganga Mkuu wa Mkoa chukua hatua Wilaya ya Rungwe hatufanyi vizuri katika Sekta ya Afya tunamuangusha Mhe.Rais Magufuli” Dkt. Ndugulile
RC MWANRI NA MADIWANI WAMEKAGUA MRADI WA BILIONI 602 “MUONDOE UMBUMBUMBU”