Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa limesema pembe ya Afrika ni eneo lililoathiriwa zaidi na uvamizi wa Nzige wa Jangwani kati ya maeneo matatu Duniani yanayokabiliwa na janga hilo.
Taarifa iliyotolewa inasema janga la Nzige limetoa tishio kubwa kwa usalama wa chakula na maisha ya Watu huku Nzige hao wakiongezeka nchini Ethiopia na Somalia na kuelekea Kusini hadi nchini Kenya.
Kwa mujibu wa FAO, operesheni za angani na ardhini zinaendelea lakini bado hazitoshi, ambapo katika kipindi cha kuzaliana kwa Nzige mwezi Februari idadi yao itaendelea kuongezeka katika nchi hizo tatu.
WAITARA AZOMEWA NA WAPINZANI BUNGENI, ISHU YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA