Leo February 5, 2020 Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Songwe, George Salala, amesema watu wanne wamefariki dunia baada ya kusombwa na mafuriko katika Wilaya za Mbozi na Ileje.
Tayari miili miwili imeshapatikana na jitihada zaidi zinaendelea kutafuta miili mingine. Inaelezwa kuwa, watatu kati ya wanne waliopoteza maisha walikuwa wa familia moja.
ACP Salala ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na kuwataka madereva kuchukua tahadhari wakati huu ambapo mvua zinaendelea kunyesha na kusababisha mito kufurika.