Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amewataka Watendaji Wakuu wa Jeshi la Polisi wawahoji watuhumiwa waliopo katika mahabusu ya Vituo vya Polisi nchini ili kujua makosa waliyoyafanya kama wanastahili kuwepo katika mahabusu hizo.
Waziri Simbachawene amesema lengo kuu la agizo hilo ni kudhibiti ubambikizwaji kesi ambao upo katika vituo mbalimbali nchini ambapo baadhi ya watuhumiwa wanapelekwa magerezani kwa makosa ambayo hawakuyafanya.
Simbachawene ameongeza kuwa, wakati mwingine mtuhumiwa anakuwa na kesi nyingine lakini anapewa kesi ya kosa ambalo hakukamatwa nalo.
Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro alimuahidi kwa kushirikiana na viongozi wenzake, watayafanyia kazi maagizo yote aliyoyatoa.
Simbachawene ameteuliwa na Rais Magufuli kuiongoza Wizara hiyo, baada ya Kangi Lugola, kuondolewa katika nafasi hiyo. Ameanza ziara ya kutembelea taasisi za wizara yake ambazo ni Jeshi la Polisi, anatarajia kufanya vikao na taasisi nyingine za wizara yake.
PROF. TIBAIJUKA AWATANGAZIA WANANCHI WAKE KUSTAAFU “SITOGOMBEA UBUNGE”