Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amezungumza na Wanahabari DSM leo Feb 29, 2020 na kusema hakuna mwenye virusi vya corona Tanzania •
“Tanzania haina mshukiwa wala mgonjwa mwenye virusi vya corona, tumejiandaa kudhibiti corona na kupambana nayo kama itaingia Tanzania, Watu zaidi ya Elfu kumi wamechunguzwa, tuna vifaa vya kupima, tumeongeza wataalamu wa afya mipakani kufuatilia”– WAZIRI UMMY
•
“Tumeimarisha uwezo wa kupima sampuli kwa wanaoshukiwa kuwa na viashiria vya corona, ndani ya masaa manne hadi sita tunaweza kutoa majibu, Wananchi wasisambaze taarifa ambazo hazijathibitishwa na Mamlaka, Serikali itaendelea kushirikiana na WHO na kutoa taarifa sahihi”- WAZIRI UMMY
EXCLUSIVE: WAZAZI WANGU WAMENITENGA KISA WANANGU WALEMAVU, BABA ANATAKA KUNIFUNGA, NIMELETA NUKSI.