James Francis Mbatia baada ya kukutana Rais Magufuli amesema pamoja na kufurahishwa na dhamira ya Rais Magufuli juu ya Uchaguzi Mkuu kuwa huru na wa haki ametaka wanasiasa waache kukamiana na kuchochea mambo hasi dhidi ya Taifa, na badala yake waungane kuendeleza mambo mazuri yanayofanywa na Serikali ikiwemo kuboresha elimu, upatikanaji wa nishati na mengine yenye maslahi mapana kwa wananchi.
Mbatia ametoa wito kwa wanasiasa na Watanzania wote kwa ujumla kuweka mbele maslahi ya Taifa badala ya kukumbatia mambo yenye maslahi binafsi, na ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kufanya vizuri katika maeneo mbalimbali licha ya kwamba wapo baadhi ya watu wanaobeza mafanikio hayo.