Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepiga marufuku Watalii wanaotokea nchini Italia ikiwa ni tahadhari za kujikinga kuingia kwa maambukizi ya Virusi Corona Visiwani humo.
Katika taarifa yake na waandishi wa habari, Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohammed amesema Serikali imefikia hatua hiyo ili kudhibiti kutokuingia kwa maambukizi hayo.
Aidha Waziri huyo amezuia kwa sherehe ya (honeymoon) iliyotarajiwa kuhusisha zaidi ya wageni 1,000 kutoka Nje ya Nchi,
Sambamba na hayo amekanusha taarifa zinazosambaa kuwa Zanzibar kumeshaanza kuingia maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo amewataka wananchi kuzipuuza na kusikiliza taarifa zinazotolewa na Serikali hivyo amezitka Taasisi husika kuwachukulia hatua watu wanaotoa taarifa ambazo sio sahihi zinazozusha kuwepo kwa maambukizi hayo.
Waziri Hamad amewataka wananchi kutoa taarifa na kumfikisha kituo cha afya mara tu watakapogundua mtu mwenye dalili za ugonjwa huo.
Ikumbukwe hapo jana Mufti Mkuu wa Zanzibar ameahirisha Ijitimai ya Kimataifa iliyotarajiwa kuanza tarehe 6 hadi 8 mwezi huu ikiwa ni hatua za kudhibiti uingiaji wa virusi corona.
UNAAMBIWA: “MKE AKIFARIKI MALI YAKE MUME HAIMHUSU” ADVOCATE SUZAN SENSO