Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amezindua kampeni ya kuthibiti maambukizi ya malaria kimkoa , kampeni hiyo imebeba ujumbe unaosema ‘Ziro Malaria inaanza na mimi’.
Kampeni hiyo imezinduliwa kimkoa katika Wilaya ya Kaliua na kwa takwimu zilizotolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honorata Rutatinisibwa, Kaliua ina Maambukizi ya Malaria kwa 16%.