Mashindano ya kuzunguka dunia baharini kwa kutumia boti zinazotumia upepo (Tanga) yamefikia Mjini Subic nchini Ufilipino yakitokea Visiwa vya Papua New Guinea ikiwa ni muendelezo wa mashindano hayo.
Akizungumza na AyoTV mshiriki kutoka Zanzibar/Tanzania Nassor El Mahruki amesema matarajio ya kufika katika Mji huo ilikuwa ni kutumia siku tisa isipokuwa kutokana na hali ya bahari kuwa mbaya imewalazimu kutumia siku kumi na moja.
“Tulitarajia kufika katika mji wa Subic kwa siku tisa ila tumechelewa na tumetumia siku kumi na moja kutokana na bahari kuwa chafu” El Mahruk
Amesema katika safari hii hakukuwa na visa vya kutisha mbali ya changamoto ndogondogo zilizojitokeza ikiwa ni pamoja na kuchanika kwa matanga kwa baadhi ya boti.
El Mahruki ameuambia mtandao wa AyoTV kuwa mbali ya kukosekana kwa visa vya kutisha katika safari yao hiyo ila washiriki watatu katika boti yao wameshindwa kuendelea na mashindano hayo na kutangaza kujiondo katika mashindano hayo.
“Tizi resi ni ngumu sana kushiriki japo waandaaji wanasema mtu yoyote anaweza kushiriki” El Mahruk