Mvutano wa maneno kati ya Marekani na China umeonekana kushika kasi huku kila mmoja akimtupia lawama mwenzake kuwa virusi vya corona vimeanzia kwenye Nchi yake, China wanasema corona haijaanzia Wuhan kama inavyoaminika bali ilianzia Marekani na Wanajeshi wa Marekani walitumika kuviingiza virusi hivyo China huku Marekani wakisema hizo ni propaganda za china tu na hazina ukweli.
Baada ya Viongozi kadhaa wa gazi za juu wa Nchi zote mbili kurushiana maneno huku Marais wakiwa hawajatoa kauli, Rais Trump amejitokeza na kusema China wanaongea uzushi unaopaswa kupuuzwa, HAPA CHINI nimekuwekea kwa urefu ripoti ya ugomvi wa China na Marekani kuhusu ilipoanzia corona.