Kesi dhidi ya Wanajeshi 27 wa zamani wa Kenya ambao walitoroka jeshini ili kujiunga na kampuni za ulinzi nchini Marekani imeanza katika kambi ya kijeshi ya Mtongwe Mombasa.
Unaambiwa Wanajeshi hawa wote walikua wakilitumikia jeshi la Kenya nchini Iraq, Afghanistan na Kuwait kati ya mwaka 2007 na 2008 na iwapo watapatikana na hatia wanaweza kufungwa jela kwa miaka miwili bila kupata nafasi ya kutozwa faini.
Inaaminika kilichowashawishi kuiacha kazi ya Serikali ni malipo makubwa pamoja na maisha yenye unafuu nchini Marekani.
Unataka usipitwe na stori kama hizi? ungana na familia ya millardayo.com kwenye twitter instagram na facebook kwa jina hilohilo la MillardAyo ili upate kila kinachonifikia iwe usiku au mchana.