Staa wa zamani wa club ya Necastle United ya England Nobby Solano amejikuta akiingia matatizoni na kupelekwa Polisi nchini kwao Peru kufuatia kudaiwa kukiuka taratibu za kujitenga (isolation).
Solano ambaye alikanusha kukamatwa na Polisi kwa sababu ya kukiuka sheria ya kujitenga na kutokaa katika mikusanyiko na makundi kama ilivyotangazwa katika nchi mbalimbali duniani aliongea na SportsMail ya UK na kuweka ufafanuzi.
“Haikuwa sherehe bali nilienda nyumba ya jirani yangu kwa ajili ya kupata chakula cha mchana na familia yangu, jirani anaishi umbali wa yadi 50 kutokea kwangu na tulikuwa watu sita, saba ilikuwa ni salama kwetu sisi wote na watoto walikuwa wanafanya mazoezi”
“Kuna mmoja alisikia sauti ya music na alijaribu kujifanya mjanja kuwaita watu wa TV, sababu za kuwa maarufu na kuwa katika macho ya watu vitu kama hivi vinaweza kutokea”