Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Uleg ametembelea mnada wa kimataifa wa Longido na mnada wa Meserani iliyopo Mkoani Arusha na kuwataka wafanyabiashara wa mifugo katika minada yote nchini kufanya biashara na kutoweka makundi huku wakifuata maelekezo ya wataalamu dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa covid 19.
Naibu Waziri Ulega ambaye pia ametoa vifaa mbalimbali vya kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona kwa Mkuu wa Wilaya ya Longido Bw. Frank Mwaisumbe amewataka wafanyabiashara kote nchini kuendelea kufanya biashara zao huku wakichukua tahadhari.