Mtandao wa mailsports wa UK umeripoti kuwa Cristiano Ronaldo ,35, ana sababu tano zitakazomfanya aendelee kuitumikia Juventus licha ya uwepo wa tetesi za kurejea Real Madrid
–
1- Urafiki wake na Rais wa Juventus Andrea Agnelli na Ronaldo anampenda sana Agnelli namna anavyoongoza timu hiyo na ukarimu wake kwa wachezaji.
–
2-PESA: Ronaldo anaingiza pesa nyingi kupitia mitandao yake ya kijamii kuliko mchezaji yoyote yule duniani, kiasi cha kuaminika kuwa pesa haitakuwa kitu cha kumshawishi sana kuondoka lakini pia mifumo ya kodi ya Italia haimbani sana mchezaji wa kigeni katika taifa hilo ukilinganisha na ilivyokuwa Hispania.
–
3-Tamaa ya kutaka kufikia rekodi ya Clarence Seedorf ambaye ndio mchezaji pekee aliyewahi kushinda UEFA Champions League akiwa na club tatu tofauti (Ajax, Real Madrid na AC Milan), Ronaldo anaamini rekodi hiyo inawezekana kwake akiwa tayari kashachukua taji hilo akiwa na Real Madrid na Man United.
–
4- Mapenzi yake katika mji wa Turin, Ronaldo inaripotiwa anafurahia mandhari nzuri ya mji wa Turin hususani katika Villa (nyumba anayoishi) Turin iko katika mazingira mazuri ya kilimani nyuma ya kanisa la Gran Madre kiasi ambacho ana nafasi ya ku-enjoy view (muonekana) wa eneo lote la Mole Antonelliana.
5- Nafasi ya uongozi, kuna tetesi zinasema kuwa Ronaldo alikuwa hafuraishwi sana na uwepo wa Mario Mandzukic katika chumba cha kubadilishia nguo sababu mchezaji huyo (Mandzukic) alikuwa na karama ya uongozi na sauti (kusikilizwa zaidi na wachezaji wenzake/watu) lakini staa huyo wa Croatia zama zake Turin zilimalizika msimu uliopita na kuondoka na sasa wamebaki Ronaldo mwenyewe, Gianluigi Buffon ,42, na Giorgio Chiellini ,35 ndio wachezaji wenye sauti zaidi.