Serikali ya Korea Kusini imesema kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un anaonekana kuendelea kuongoza shughuli za Serikali kama kawaida, baada ya uvumi usio na uthibitisho kusema kuwa yuko katika hali dhaifu baada ya kufanyiwa upasuaji.
Ikulu ya Korea Kusini imesema hakuna tukio lolote lisilo la kawaida ambalo limegundulika Korea Kaskazini na kuwa haina habari yoyote kuhusu uvumi huo kuhusu afya ya Kim.
Ikulu ya Korea Kusini imesema Kim anaaminika kuwa katika eneolisilojulikana nje ya mji mkuu wa Pyongyang akiwa na Watu wake wa karibu.
Katibu wa Baraza la mawaziri la Japan Yoshihide Suda amesema wanafuatilia habari hizo kwa karibu.
Imeandikwa na Idhaa ya Kiswahili
WABUNGE WALIVYOELEZA MASIKITIKO YAO KIFO CHA MAMA RWAKATARE