Leo naomba nikusogezee list ya wachezaji soka saba ambao kwenye maisha yao ya soka wamewahi kufanya majaribio na kukataliwa na baadhi ya vilabu na baadae kuibuka na kuwa wachezaji wakubwa duniani.
7- Inawezekana Mario Balotelli tungewahi kumuona akiichezea FC Barcelona lakini ndio hivyo haikutokea, hii inatokana na staa huyo wa soka kuwahi kufanya majaribio katika timu ya vijana ya FC Barcelona akiwa na umri wa miaka 16 na kufuzu, mkuu wa timu ya vijana wa Barcelona wa wakati huo Jose Ramon Alexanko alipenda uwezo wake lakini baadae waliachana nae sababu ya nidhamu.
6- Diego Costa wa Atletico Madrid wengi wanamfahamu kama mchezaji ambaye ana hasira za haraka hawapo uwanjani, alipokuwa kwao Brazil alikuwa akicheza soka mtaani pasipokuwa na kocha wa muongozo wowote hadi alipofikia umri wa miaka 15, Diego Costa alitafutiwa nafasi kujiunga na club za Brazil za Corinthians, Palmeiras na Santos na baadae kwenda Ulaya na kupokelewa na club ya Braga na soka lake kuanzia pale.
5- Mshambuliaji wa Man United Marcus Rashford wakati akiwa na umri wa miaka 9 aliwahi kufanya majaribio katika club ya Man City na kukataliwa kwa kigezo kuwa alikuwa na umbo dogo na dhaifu wakiamini hawezi kuwa na msaada katika timu, hapo ndipo alipotafuta nafasi nyingine na kuipata katika timu za vijana za Man United na leo hii anasumbua safu ya ushambuliaji ya Man United na kuipa stress Man City pale ambapo wanakutana na Man United.
4- Mshambuliaji Harry Kane ambaye anaongoza safu ya ushambuliaji ya Tottenham naimani hakuna asiyemjua kutokana na umahiri wake wa kucheka na nyavu pale tu inapotokea kapokea pasi akiwa na Spurs na hata timu yake ya taifa ya England, Kane aliwahi kukataliwa na Arsenal baada ya kuwa katika academy Highbury ya Arsenal wakati huo kwa mwaka mmoja lakini kocha wa Arsenal Arsene Wenger ilidaiwa kuwa alimpiga chini kutokana na umbo lake kuwa mdogo na kibonge sana.
3- Kiungo wa zamani wa Man City na timu ya taifa ya Ivory Coast Yaya Toure akiwa na umri wa miaka 20 mwaka 2003 aliwahi kufanya majaribio katika club ya Arsenal na kucheza mechi za kirafiki za maandalizi ya msimu mpya lakini kocha wa Arsenal wa wakati huo Arsene Wenger alimkataa na kusema kuwa uwezo wake ni wastani tu sio wa kumvutia, hivyo akaenda kujiunga na club ya Metaruh Dotsk ya Ukraine na baada akajiunga na vilabu vya FC Barcelona na akarejea England katika club ya Man City na kuandika rekodi ya mchezaji anayelipwa zaidi EPL kwa wakati huo.
2- Ukitaja wachezaji bora wa nafasi ya ushambuliaji waliwahi kutokea mwishoni mwa karne ya 20 na mwanzoni mwa karne ya 21 basi huwezi kuacha kumtaja Ronaldo Luis Nazario Delima huyu ni binadamu anayetajwa kuwa na jicho na goli anajua kufunga, football commentator wengi duniani wamewahi kumpamba kwa majina mbalimbali, Ronaldo aliwahi kukataliwa na club ya Flamengo ya kwao Brazil lakini haikuwa shida akapata nafasi ya kujiunga na club ya Cruizero na kwenda kufunga magoli 44 katika mechi 47 na kuondoka zake kwenda Ulaya PSV Endhoven ya Uholanzi akiwa na miaka 17 alipotimiza miaka 18 akaweka tena rekodi ya kufunga magoli 51 katika michezo 54.
1- Kwa miaka takribani sita Lionel Messi alikuwa katika academy ya Newell Old Boys ya nchini kwao Argentina, akiwa na umri wa miaka 12 club ya River Plate ya nchini kwao Argentina ambao ni kama Simba au Yanga ya Argentina, ilimkataa baada ya kujua kuwa mchezaji huyo atawagharimu pesa nyingi kumtibia ndipo, Messi ambaye alikuwa na tatizo la ukuaji alitakiwa kila mwezi alipiwe dola 1000 (Tsh milioni 2.4) ili kununuliwa dawa za kusisimua homoni zake za ukuaji, gharama hizo River Plate hawakutaka kuziingia ndipo FC Barcelona wakakubali na kumchukua na kumpeleka La Masia hadi leo hii Messi ni shuja wao pale Nou Camp na miongoni mwa wachezaji bora kuwahi kutokea duniani na tajiri.