Dar es salaam imekua ikipokea mvua kubwa sana kwenye siku hizi za karibuni ambayo imehusika sana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kwa watu kuonyesha jinsi madimbwi yalivyotawala hata kwenye sehemu ambazo hazikutarajiwa barabarani.
Ukubwa wa hizi mvua ulisababisha ukungu mkubwa sana April 11 2014 mchana wakati ndege ya shirika la Kenya na abiria 49 ikiwa inatua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam ikitokea Kenya.
Marubani walipata tabu wakati wa kutua hivyo ikatua kwa kishindo kilichopelekea ishindwe kutua kwenye barabara kama inavyotakiwa na badala yake ikaingia mpaka kwenye majani.
Polisi ilipozungumza na Radio One, imesema ajali hiyo ilisababisha kusitishwa kwa safari zote za ndege kuondoka na kutua huku abiria waliokuwemo ndani ya hii wakishushwa kwa dharura kama moja ya hizi picha inavyoonyesha hapo chini mwisho.
Sehemu ya injini ya upande wa kulia ya ndege hii iliyokua na Wafanyakazi saba ndani yake, imeharibika kutokana na kukita chini kwa kishindo wakati wa kutua.
Hakuna yeyote aliepoteza maisha isipokua kuna taarifa chache za waliopata majeraha kidogo kwenye ngazi wakati wakishuka kwa dharura kama inavyoonekana kwenye picha ya mwisho chini.
Unataka kila tukio linalonifikia niwe nakutumia? karibu ujiunge na familia ya millardayo.com kwenye twitter instagram na facebook kwa jina hilohilo la MillardAyo.