Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa, idadi ya wagonjwa wa Corona hapa nchini imepungua kwa kiasi kikubwa na kubaki na wagonjwa wanne pekee walio katika Mkoa wa DSM.
Waziri Ummy ameyabainisha hayo leo June 1, 2020, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ya uzinduzi wa jengo la Bodi ya Mkonge lililopewa jina la Mkonge House, na kusisitiza kuwa kwa takwimu hizi watu wasijisahau, bali waendelee kujikinga na ugonjwa huo.