Wizara ya Ulinzi ya India imetia saini kununua ndege 33 za kijeshi kutoka Urusi na 59 nyingine kuzifanya za kisasa zaidi zenye thamani ya Dola Bilioni 2.4, huku kukiwa na ongezeko la hali ya wasiwasi na nchi jirani ya China yenye silaha za kinyuklia.
Ununuzi wa ndege chapa MiG-29 na 12 SU-30 MKI, pamoja na ukarabati wa ndege nyingine 59 chapa MiG-29, ilikuwa kuweka sawa uwezo wa jeshi la anga la India, wizara ya ulinzi imesema.
Mifumo mipya na ya ziada ya makombora itakayotengenezwa nchini India pia imenunuliwa kwa vitengo vyote vitatu vya jeshi la India.
Ongezeko la uwezo wa ulinzi nchini India ulichukuliwa kutokana na haja ya kuimarisha majeshi ya ulinzi ili kulinda mipaka ya nchi hiyo na wito wa waziri mkuu Narendra Modi wa India inayojitegemea, wizara hiyo imeongeza katika taarifa.