Serikali Wilayani Hai imeondoa zuio batili lililowekwa na baadhi ya Viongozi katika Kijiji cha Isuki Kata ya Masama Kati ambalo lilikuwa linakataza Wananchi kutembea na kutokwenda Bar kuanzia saa mbili usiku.
Mkuu wa Wilaya Hai Lengai Ole Sabaya ameiongoza Kamati ya Usalama na kuamuru Viongozi watano wa Kijiji hicho kushikiliwa na Vyombo vya dola kwa kuwatoza wananchi kiasi cha Elfu sitini au kuwachapa viboko na kuwapaka upupu kwa walioshindwa kutekeleza amri hiyo batili.
Katika hatua nyingine amesitisha shughuli za sungusungu na kuamuru kuondolewa kwa Polisi Kata kwa kushindwa kulinda wananchi na mali zao huku akinyamazia uonevu na unyanyasaji.