Hizi ni ripoti kutoka Arusha mjini, Watu bado wanaendelea kuweka wazi nia zao za kuomba ridhaa za kugombea nafasi za Ubunge ambapo kwenye post hii, Muhusika ni Mwanasheria maarufu Albert Msando ambaye leo amechukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)
Baada ya kuchukua fomu hiyo Msando ambaye amewahi kufanya kazi na Watu mbalimbali wakiwemo Wasanii Ay, MwanaFA na Wema Sepetu amesema “nawashukuru wote ambao mmenipa moyo na kunitakia kheri, safari hii inapaswa kuwa ya pamoja”
Saa 16 kabla ya kuchukua fomu, Msando pia aliandika “Ahsante Mungu, sasa niko tayari ksho tarehe 15/07/2020 saa nne asubuhi nitachukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama changu kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Arusha Mjini, kwanini na nini nitafanya nimeeleza kwenye Dira Yangu 2020/2025 ambayo nitaiweka wazi baada ya kurudisha fomu na muda wa kufanya kampeni kufunguliwa rasmi”
“Ninachokiamini, uchaguzi huu ni wa Vijana na kwa ajili ya vijana, rai yangu ni kufanya siasa isiyo na chuki wala vurugu, kesho ya kila mmoja wetu ni bora zaidi, tunaweza kupingana mawazo, mtazamo au itikadi bila chuki na kuongozwa na upendo, tushindanishe hoja, tuweke mahitaji ya Wananchi mbele, kuwa Chama tofauti isiwe sababu ya kupandikiza chuki na utengano ndani ya Jiji la Arusha na Tanzania kwa ujumla, sisi ni Watanzania, Mimi na wewe” – Msando.
MAAJABU: DUKA LISILO NA MLANGO WA MBAO WALA WA CHUMA NA HAKUNA ANAYETHUBUTU KUIBA KITU
KUTANA NA MWALIMU MAPROSOO, ANAEFANYA BIASHARA BAADA YA KUFUNDISHA