Idadi ya watia nia inazidi kuongezeka ambapo kwa uchaguzi mkuu wa October mwaka huu idadi ya Watu maarufu waliotangaza nia imekua kubwa pengine kuliko miaka iliyopita, mwingine ambae amechukua fomu ni Miss Tanzania Lilian Kamazima.
Lilian ambae alikuwa Miss Tanzania 2014 amechukua fomu ya kugombea Ubunge wa Viti maalum Mkoa wa Arusha ambako ndiko anakotokea, pia kabla ya kugombea Ubunge huo Lilian amekua akijishughulisha na harakati za utetezi na kumkomboa Mwanamke.
Lilian anaingia kwenye orodha ya Watu wengine maarufu waliochukua fomu kugombea Ubunge kwenye maeneo mbalimbali Tanzania ambapo wengine ni pamoja na Producer Master J, Babu Tale, Steve Nyerere, Mwandishi Baruani Muhuza, MC Pilipili, Msanii Kalapina, Rapper Wakazi, Mtangazaji Harris Kapiga na wengine.