Urusi yatarajia kupunguza matumizi kwa jeshi lao kwa 5% kwa mwaka 2021 hadi 2023 kutokana na kupungua kwa bei za mafuta na janga la COVID19 lilivyoathiri uchumi wa nchi hiyo.
Kwa takwimu za mwaka 2019 Urusi ilikuwa ni nchi ya nne kwa matumizi makubwa ya jeshi, pesa iliyokuwa ikitumika ilikuwa ni 3.9% ya Pato la Taifa.
Rais Vladimir Putin amehitaji kuboresha maisha ya watu na kuwekeza katika Afya na Elimu, viongozi wengine walishauri apunguze matumizi kwa Jeshi ili kufanikisha hayo
Imesemekana kwamba matumizi katika Jeshi yamekuwa yakiongezeka tangu Rais Putin aingie madarakani, japo taarifa kuhusu kiwango cha pesa kinachotumika kwa matumizi ya jeshi kinasemwa kuwa ni siri ya nchi.