Marekani imeitaka China kufunga ubalozi wake mdogo katika Jiji la Texas katika Jimbo la Houston, Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema ikilaani vikali uamuzi huo na kutishia kuchukua hatua za kulipiza kisasi.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wang Wenbin, amesema Beijing iliarifiwa ghafla kuhusu hatua hiyo Jumanne wiki hii, hata hivyo hakutoa sababu za Marekani kuitaka China kufunga ubalozi wake mdogo huko Texas.
Mamlaka nchini Marekani imeipa China siku tatu kuwa imefunga ubalozi wake mgodo Texas, Wang Wenbin amesema.
“Hatua ya Marekani kufunga ubalozi wa China huko Houston, bila hata hivyo kuishirikisha serikali ya Beijing, katika kipindi kifupi kama hiki ni muendelezo wa hatua za hivi karibuni za Marekani dhidi ya China,” Wenbin
“Tunaiomba Marekani kufuta uamuzi huo mbaya mara moja. Kama itaendelea kushikilia uamzi wake huo mbaya, China italipiza kisasi kwa kuchukuwa hatua kali, “Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China.