AyoTV mwaka jana iliweka kambi nchini South Africa huko Pretoria lengo lilikuwa ni kufanya mahojiano na Mrembo, Mjasiriamali Zari The Boss Lady akazungumza mengi kuhusu yakiwemo mahusiano yake na mengineyo.Sasa leo tumekusogezea mwendelezo wa nyumba aliyokuwa akiishi na mumewe Ivan yakiwemo na magari ya thamani.
Akizungumza na Ayo TV Zari The Boss Lady alifunguka na kusema ‘Hii nyumbani tulinunua kitambo sana lakini tulipoachana Ivan akaamua kuniachia hii nyumba mnayoiona hapa na wakati huo alikuwa ni mtu ambae alikuwa anakuja kuwachukua watoto na kuondoka na kuwarudisha’-Zari The Boss Lady
‘Hizi mali tulitafuta kwa pamoja na Ivan, haya magari unayoyaona yatatumiwa na watoto wetu huko mbeleni kwahiyo nashangaa watu wakiongea wasichokijua kuhusu mimi na Ivan’- Zari The Boss Lady