Leo August 12, 2020 nakukutanisha na Dada Flora ambaye anatusimulia mambo mbalimbali aliyokutana nayo katika maisha yake ikiwemo kupata ajali Mkoani Manyara yeye pamoja na Mumewe muda mfupi baada ya kutoka kufunga ndoa.
“Baada ya kumaliza kupiga picha ilitakiwa tusafiri kuelekea Babati, nilisita kwenda Babati wifi yangu akanitalia akasema lazima twende wote ikabidi nikubali nikaenda kubadilisha nguo nikavaa nguo za kawaida tukaanza safari” Dada Flora
“Tukiwa njiani ilitakiwa tukate kona ile tunakata kona nilisikia mlio paaah, nikawa nahisi gari ina biringika, Mume wangu alikua kama anatoka usingizini akauliza kuna nini nikamwambia ni ajali ilikuwa ni Saa 3 usiku” Dada Flora
“Walianza kuvuta gari kila ikuvutwa tunaumia, wakaanza kuikata na shoka ili watutoe, katika ajali ile walifariki watu saba mimi na Mume wangu tulipona” Dada Flora